Kiama Chao by Philipo Oyaro

Kiama Chao

byPhilipo Oyaro

Kobo ebook | April 21, 2017

Pricing and Purchase Info

$3.93

Prices and offers may vary in store

Available for download

Not available in stores

about

Rose Simon anakuwa mjane baada ya kuuawa kwa mumewe, Julius Mabala, mwanaharakati aliyekuwa amejitolea maisha yake kupambana na rushwa na ufisadi--akiwa amejiridhisha pasipo shaka yoyote yuko tayari kuwasilisha tuhuma na ushahidi na pia kushirikiana na vyombo husika katika kuhakikisha kuwa sheria inafuata mkondo wake.

Akiwa mbele ya kamera za televisheni, muda mfupi tu baada ya mazishi ya Julius, Rose anatoa tamko linalowatia kiwewe wauaji wa Julius. Siku chache baadaye akiwa safarini gari lake linagongwa na gari jingine. Waliomgonga wanapoondoka eneo la tukio wanaamini kuwa wamemaliza kazi. Vyombo vya habari havikuripoti taarifa hii. Ndugu na jamaa wanamtafuta bila ya mafanikio.

Kwa miezi kadhaa anatibiwa hopitalini hapo huku madaktari na wauguzi wakiwa wamekata tamaa lakini katika  kama muujiza afya yake inaimarika.

Anaporejea Jijini Dar es Salaam anakuwa na jambo moja tu kichwani--kuendeleza kazi aliyoiacha Julius. Hili linamuingiza katika mshikemshike kwani harakati hizo zinagusa vigogo ambao wamewekeza kwa kiasi kikubwa katika kuyasaka mamlaka ya juu ya uongozi wa nchi; vigogo ambao hawako tayari kuona ndoto zao za kutafuna keki tamu ya taifa hili ikiwaponyoka. Harakati hizi zinakuwa sawa na kujipalia makaa. Yeye na watu wake wa karibu hawako salama. Vigogo hao wamenuia kuwafutilia mbali hivyo kusababisha damu zaidi kumwagika.

Title:Kiama ChaoFormat:Kobo ebookPublished:April 21, 2017Publisher:Philipo Oyaro

The following ISBNs are associated with this title:

ISBN:9990052792705

Look for similar items by category:

Reviews